Sunday, June 1, 2014

MR. BROWN NYANZA (Chief Coordinator and Executive Director of TANZANIA SMARTPHONES FORUM) Invites local and International sponsors around the Globe:

Tanzania Smartphones Forum is an open platform for both gadgets users and business professionals who based in Tanzania and Africa in General, This forum will provide an excellent opportunity to network and exchange business ideas relating to the product and services relating to smart gadgets in Tanzania. Tanzania smartphones forum will provide a special opportunity to all companies to promote their products, technology and services; also will create effective partnership with Tanzanians researches, civil society, policy makers and development communities. 

We kindly invite sponsors all over Tanzania, Africa and all over the World at Large:
Contact us: Via
Cell; + 255 718 282874
E-Mail #1: emarketingtz@gmail.com
E-Mail #2: Brojustnyanza@gmail.com

"Join us, and be Connected to worlds Greats Innovative Mind"

Thursday, May 29, 2014

DILI YA APPLE NA BEATS AUDIO YAKAMILIKA RASMI

Picha ya pamoja Dr. Dre, Jim lovine, Mr Cook na Mr. Cue

Friday, May 23, 2014

Saturday, May 10, 2014

TANZANIA COLLEGE FESTIVALS 2014


 SOON ON 
17 MAY 2014
STAY TUNED
MZUMBE UNIVERSITY MBEYA CAMPUS COLLEGE.

APPLE YAZIDI KUONGEZA THAMANI, SASA YAINUNUA BEATS AUDIO

Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali, Kampuni ya Apple imetangaza dili ya kununua kampuni ya Beats by dre kwa jumla ya DOLA BILIONI 3.2  ($3.2 BILIONS), Kampuni ya Beats inamilikiwa na msanii nguli wa HipHop Dr. Dre pamoja na mwanzilishi wa Interscope Jimmy Lovine.

Thursday, April 17, 2014

MZUMBE UNIVERSITY MBEYA CAMPUS COLLEGE; TECHNOLOGY WEEK


  Prepared by Brown Nyanza, Sooon this Year;

Sunday, March 9, 2014

GOOGLE SMARTWATCH

Google SmartWatch. Kampuni ya google imetoa Idea ya saa mpya ya kisasa, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kongwe katika ulimwengu wa Tehama ilitanguliwa na #SamsungGear kutoka kampuni ya samsung electronic na #iWatch kutoka kampuni ya Apple Inc




Saturday, August 3, 2013

KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI MAZURI YA MAWASILIANO

Habari kwa niaba blog ya MAISHA NA TEKNOHAMA
 
Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.

Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.

Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.

Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.
 
Julai 31,2013 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.

Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.

Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
31 Julai 2013
 

SONY NA PANASONIC WAUNGANA KUTEGENEZA CD YENYE UWEZO WA HIFADHI GB 300.

 Tarehe 29/07/2013, Kampuni mbili maarufu duniani SONY Corporation na PANASONIC Corporation kupitia tovuti zao wametangaza kuwa wameingia katika makubaliano ya kutengeneza CD (compact disk/Optical Disc) zenye uwezo wa kuhifadhi GB 300 za data ifikapo mwaka 2015.
 
Kampuni zote mbili zimeongeza kwa kusema kwamba hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya CD duniani. Katika miaka ya karibuni CD zimesifika kuwa na uwezo wa kuhifadhi data kwa ulizi wa hali ya juu, hii ni kutokana uwezo mkubwa wa kuhimili  mabadiliko mbalimbali ya kimazingira, vumbi, joto, na pia CD inaweza kuhifadhi  data kwa kipindi kirefu sana iwapo ikihifadhiwa sehemu nzuri.
 
Kampuni hizo zimekaririwa kwa kusema kwamba wateja wao hasa wamelengwa kuwa makampuni makubwa ya kutengeneza filamu nchini marekani na duniani kote, Pia makampuni makubwa ya utangazaji, Pia (Cloud based Data centes) zinatarajiwa kuwa ndio soko kubwa katika teknolojia hii mpya ya kuhifadhi data. Katika miaka ya karibuni Kampuni ya SONY ilitengeneza CD zenye zinazotumia teknolojia ya BluRay zenye uwezo wa kutunza data kwa kiasi cha GB 25 hadi GB 50 katika CD moja tu.
 

Friday, August 2, 2013

HISTORI YA SMS KWA UFUPI

Na Millard Ayo.(Mwandishi/Mtangazaji Clouds Media)
Ni uhakika yani kwa wakati huu ni mara chache sana watu kutokea kukumbuka tulipotokea kwenye hizi simu za mkononi, ni rahisi kusahau manake kwa sasa kila baada ya muda mfupi utasikia tu kampuni flani ya simu imetangaza toleo jipya la simu ambalo sijui ina internet, unaweza kuwasiliana kwa video na mengine hayo.
Ni rahisi pia kusahau au inawezekana ulikua hujui kabisa, msg ya kwanza (sms) kwenye simu ya mkononi duniani ilianza kutumwa December 3 1992 na ilikua na maneno mafupi yasemayo “Merry Christmas”
Unaambiwa the first text ilitoka kwenye PC kwenda kwenye mobile device over Vodafone’s U.K ambapo aliyegundua ni bwana Matti ambae hata hivyo hajawahi kutengeneza pesa yoyote kutokana na hiyo idea ambayo alianza kuiongelea kwenye mkutano uliohusu mawasiliano mwaka 1984 .
Matti anakubali kwamba wengine ndio wameiendeleza au kuikuza hiyo idea yake ya sms ambapo pamoja na hilo, anaamini kwamba teknolojia ya sms ilizinduliwa mwaka 1994 wakati Nokia unveiled its 2010 mobile phone, device ya kwanza ambayo iliweza kusaidia watu kutuma msg kiurahisi.


Monday, July 29, 2013

TECH EVOLUTION

 
This is 1956. And this is a 5 Megabyte disk owned by IBM being loaded into the plane. It weighed 1,000 kilograms. Today, we carry 5MB disks in our wallets.
 
This post is courtesy of
Deputy Minister of Communication, Science and Technology
Hon. January Makamba.
 

Sunday, July 28, 2013

"GOOGLE PLAY" NDIYO APP STORE KUBWA ZAIDI DUNIANI IKIWA NA JUMLA YA PROGRAMU TUMISHI MILIONI MOJA.

Kampuni ya Google mapema wiki hii katika tukio la kuzindua kifaa chake cha chromecast  na tabiti yake mpya ya Nexus 7, Imetoa takwimu ambazo zinaiweka Application store ya “Google play” kuwa ndio App store kubwa zaidi duniani ikiiacha nyuma App store ya Kampuni pinzani kibiashara ya Apple inayojulikana kwa jina la Apple’s app store. “Google play” Ina jumla ya program tumishi (applications) zaidi ya milioni moja, Wakati Apple’s App store ina jumla ya program tumishi laki tisa. Programu tumishi hizo ni pamoja na vitabu vya mtandao (digital books), games, vipindi vya televisheni na mengineyo mengi.