Friday, July 26, 2013

KALAMU YA KUGUNDUA MAKOSA

Wanasayansi wawili katika nchi ya Ujerumani wamegundua kalamu inayotoa alama pindi mwandishi anapokosea herufi “spelling error.” Kalamu hiyo imepewa jina la Lernstift neno la kijerumani linalomaanisha learning pen, Yaani kalamu ya kusomea ama kujifunzia.
 Katika mahojiano maalumu katika kituo cha CNN, Mmoja ya Wanasayansi hao alisema wazo la kalamu hiyo limekuja baada ya kuona mke wake akikasirika mara kwa mara pindi anapomuona mtoto wao akihangaika kwa kukosea  herufi kila mara wakati wa kufanya mazoezi ya nyumbani (homework), Ndipo akasema kwa hasira “kwanini kusiwe na peni inayotoa alama fulani pindi mtoto anapokosea herufi wakati wa kuandika.” Ndipo mawazo ya mumewe yakaenda mbali zaidi na kufikiria kuteneneza peni hiyo iliyoleta gumzo katika vyombo vya habari mbalimbali  duniani kila kukicha. 
 Kalamu hiyo hutoa alama kwa kutetemeka  yaani “vibration” pindi unapokosea herufi wakati wa kuandika. Kwa sasa kalamu  hiyo inagundua lugha mbili tuu, kingereza na kijerumani, pia unaweza kuunganisha na Smartphone yako, tabiti (tablet) au computer na kuona kitu unachokiandika katika karakasi.

 



 

 





1 comment:

Anonymous said...

hongera sana brown