Tarehe
29/07/2013, Kampuni mbili maarufu duniani SONY
Corporation na PANASONIC Corporation kupitia tovuti zao wametangaza kuwa wameingia
katika makubaliano ya kutengeneza CD (compact disk/Optical Disc) zenye uwezo wa
kuhifadhi GB 300 za data ifikapo mwaka 2015.
Kampuni
zote mbili zimeongeza kwa kusema kwamba hii itakuwa ni mara ya kwanza katika
historia ya CD duniani. Katika miaka ya karibuni CD zimesifika kuwa na uwezo wa
kuhifadhi data kwa ulizi wa hali ya juu, hii ni kutokana uwezo mkubwa wa
kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kimazingira,
vumbi, joto, na pia CD inaweza kuhifadhi data kwa kipindi kirefu sana iwapo
ikihifadhiwa sehemu nzuri.
Kampuni
hizo zimekaririwa kwa kusema kwamba wateja wao hasa wamelengwa kuwa makampuni
makubwa ya kutengeneza filamu nchini marekani na duniani kote, Pia makampuni
makubwa ya utangazaji, Pia (Cloud based Data centes) zinatarajiwa kuwa ndio
soko kubwa katika teknolojia hii mpya ya kuhifadhi data. Katika miaka ya
karibuni Kampuni ya SONY ilitengeneza
CD zenye zinazotumia teknolojia ya BluRay zenye uwezo wa kutunza data kwa kiasi
cha GB 25 hadi GB 50 katika CD moja
tu.
No comments:
Post a Comment